Friday, July 12, 2013

MASOGANGE AMEKAMATWA


HUKU skendo ya kunaswa akiwa na madawa ya kulevya ikiendelea kumtesa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, Video Queen maarufu Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ anatarajiwa kupandishwa kortini nchini Afrika Kusini leo kujibu shitaka ambalo mwenyewe hajaliweka wazi

Thursday, June 27, 2013

Ally Mzich Akiwa na Dj Choka

Mmoja Kati ya Waasisi Wanaounda Kundi la Muziki wa Hip Hop (Mazich Reality) Mjini Dodoma.
Kushoto Ally Mzich akiwa Dj Choka, Katika Ma Dj Bora Nchini Tanzania na Afrika Yote

ASKOFU THABO MAKGOBA AFANYA MAOMBI MAALUM KWA AJILI YA MANDELA


Askofu mkuu wa kanisa la kianglikana mjini Cape Town, Afrika Kusini, Thabo Makgoba, amejitolea kufanya maombi kwa niaba ya rais mstaafu Nelson Mandela ambaye anaugua sana hospitalini.
Kasisi huyo anamuombea Mandela aweze kupata nafuu na amewataka wananchi kumshukuru kwa yote aliyowafanyia.
Jamaa za Nelson Mandela wamekutana nyumbani kwake huko Kunu, huku hali yake ya afya ikizidi kudorora hospitalini, Pretoria.
Afya ya Bwana Mandela ilikuwa mbaya zaidi Jumapili.
Maombi hayo yalitolewa baada ya Askofuu huyo kumtembelea Mandela hospitalini ambako kiongozi huiyo wa zamani amekuwa akilazwa kwa wiki mbili na nusu zilizopita baada ya kuugua mapafu.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa wajukuu wa rais huyo wa zamani wa Afrika kusini wanakutana nyumbani kwake kijijini katika mkoa wa Eastern Cape province, ambako viongozi wa kitamaduni wamealikwa.
Halikopta ya jeshi kadhalika zilionekana zikipaa karibu nyumbani kwa mandela. Afisi ya Rais jacob Zuma ilitangaza jumapili kuwa hali ya mzee Mandela ya afya ilikuwa mbaya sana.

UJIO WA RAIS BARAKA OBOMA NCHINI TANZANIA


Rais wa Marekani Bw. Baraka Obama na Mkewe wanatarajia kufanya ziara ya nchi tatu barani Afrika itakayojumuisha nchi za Senegal, Afrika ya Kusini na Tanzania, Kuanzia tarehe 26 Juni hadi tarehe 3 Julai. 
Katika ziara yake hiyo, Rais atawekea mkazo umuhimu ambao Marekani inauweka katika ushirikiano wetu wa kina na unaoendelea kuimarika na nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia mipango mbalimbali ikiwemo ile ya kuimarisha ukuaji wa uchumi, uwekezaji na biashara, uimarishaji wa taasisi za kidemokrasia na uwekezaji katika kizazi kipya cha viongozi wa Kiafrika.
Rais atakutana na viongozi mbalimbali wa kiserikali, sekta binafsi na jumuiya huru ya kiraia ikiwemo vijana ili kujadili ubia wetu wa kimkakati katika ushirikano wetu rasmi na masuala mengine ya kimataifa.
 
Ziara hii itadhihirisha dhamira ya dhati ya Rais ya kupanua na kuimarisha ushirikiano kati ya Marekani na watu wa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara katika kuimarisha amani na ustawi katika kanda hii na duniani kote kwa ujumla

Wednesday, June 26, 2013

Hali ya wasiwasi kuhusu afya ya Mandela

Wananchi wa Afrika Kusini  wamekuwa na wasiwasi baada ya rais wa nchi hiyo Jacob Zuma kutangaza kuwa hali ya afya ya rais mstaafu Nelson Mandela sio nzuri sana.
Asubuhi waliamkia kwenda kazini wasijue taarifa watakazopokea  baada ya rais Zuma kutoa taarifa hiyo.
Taarifa kutoka ikulu ya rais zilisema Jumapili jioni kuwa Mandela alikuwa amezidiwa ingawa madaktari wanafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa anapata afueni.
Afisaa mmoja mkuu alisema kuwa raia wa Afrika Kusini wasiwe na matumaini kupita kiasi.
Mandela ambaye alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, akiwa na umri wa miaka 94,alipelekwa hospitalini mapema mwezi huu, ikiwa ni mara ya tatu kwake kulazwa hospitalini akiugua ugonjwa wa mapafu mwaka huu.
Rais Jacob Zuma alisema Jumapili kuwa alimzuru Mandela Hospitalini na kuzungumza na mkewe kuhusu hali ya rais mstaafu.
Madaktari wanaomtibu Mzee Nelson Mandela wamesema hali yake imekuwa sio nzuri kwa saa ishirini na nne zilizopita na sasa ni mahututi.
Habari hizo zimekuja kupitia taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais ya Afrika Kusini.
Taarifa hiyo imesema bado Mzee Mandela ameendelea kusalia hospitalini mjini Pretoria kwa siku ya kumi na sita akitibiwa mapafu yaliyosababisha tatizo kwenye mfumo wake wa upumuaji.
Rais Jacob Zuma amemtembelea Mzee Mandela na pia kuzungumza na jopo la matabibu wanaomtibu.
Baadaye bwana Zuma alirejea kauli yake ya kulitaka taifa na dunia kumuombea Mzee Mandela apate nafuu.